22 Na maji hayo yamekuwa ya kufaa mpaka leo, kama alivyosema Elisha.
23 Elisha aliondoka Yeriko, akaenda Betheli. Alipokuwa njiani, vijana fulani walitoka mjini wakaanza kumzomea wakisema, “Nenda zako, nenda zako mzee kipara!”
24 Elisha aligeuka akawatazama na kuwalaani kwa jina la Mwenyezi-Mungu. Dubu wawili majike wakatoka mwituni, wakawararua vijana arubaini na wawili miongoni mwao.
25 Elisha akaendelea na safari yake mpaka mlima Karmeli na kutoka huko akarudi Samaria.