29 Tukampika mwanangu, tukamla. Kesho yake nikamwambia tumle mwanawe, lakini alikuwa amemficha!”
30 Mara mfalme aliposikia maneno ya mwanamke huyo alirarua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa vazi la gunia ndani yake.
31 Naye akasema, “Mungu aniue, Elisha mwana wa Shafati asipokatwa kichwa leo!”
32 Ndipo akatuma mjumbe kwenda kumleta Elisha.Wakati huohuo Elisha alikuwa nyumbani pamoja na wazee waliomtembelea. Kabla ya mjumbe wa mfalme kufika, Elisha akawaambia wazee, “Yule muuaji amemtuma mtu kuja kunikata kichwa! Atakapofika hapa, fungeni mlango, wala msimruhusu aingie. Pia bwana wake anamfuata nyuma.”
33 Kabla hata hajamaliza kusema, mfalme akafika, akasema, “Msiba huu umetoka kwa Mwenyezi-Mungu! Kwa nini niendelee kumngojea tena?”