12 Lakini nyinyi mliwafanya wanadhiri wanywe divai,na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13 “Sasa basi, nitawagandamiza mpaka chini,kama gari lililojaa nafaka.
14 Hata wapiga mbio hodari hawataweza kutoroka;wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,na askari watashindwa kuyaokoa maisha yao.
15 Wapiga upinde vitani hawatastahimili;wapiga mbio hodari hawataweza kujiokoa,wala wapandafarasi hawatayanusurisha maisha yao.
16 Siku hiyo, hata askari hodariwatatimua mbio bila chochote.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”