8 Popote penye madhabahu,watu hulalia nguo walizotwaa kwa maskinikama dhamana ya madeni yao;na katika nyumba ya Mungu waohunywa divai waliyotwaa kwa wadeni wao.
9 “Hata hivyo, enyi watu wangu,kwa ajili yenu, niliwaangamiza kabisa Waamoriambao walikuwa wakubwa kama mierezi,wenye nguvu kama miti ya mialoni.Naam, niliwaangamiza, matawi na mizizi.
10 Niliwatoeni kutoka nchi ya Misri,nikawaongoza kupitia jangwani miaka arubaini,mpaka mkaichukua nchi ya Waamori kuwa yenu.
11 Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii,na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri.Je, enyi Waisraeli,haya nisemayo si ya kweli?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12 Lakini nyinyi mliwafanya wanadhiri wanywe divai,na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13 “Sasa basi, nitawagandamiza mpaka chini,kama gari lililojaa nafaka.
14 Hata wapiga mbio hodari hawataweza kutoroka;wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,na askari watashindwa kuyaokoa maisha yao.