1 Enyi Waisraeli, sikilizeni neno Mwenyezi-Mungu alilosema dhidi yenu, enyi taifa zima alilolitoa nchini Misri:
2 “Kati ya mataifa yote ulimwenguni,ni nyinyi tu niliowachagua.Kwa hiyo nitawaadhibu nyinyi,kwa sababu ya uovu wenu wote.”
3 Je, watu wawili huanza safari pamoja,bila ya kufanya mpango pamoja kwanza?
4 Je, simba hunguruma porinikama hajapata mawindo?Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwakekama hajakamata kitu?
5 Je, mtego bila chamboutamnasa ndege?Je, mtego hufyatukabila kuguswa na kitu?