3 Je, watu wawili huanza safari pamoja,bila ya kufanya mpango pamoja kwanza?
4 Je, simba hunguruma porinikama hajapata mawindo?Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwakekama hajakamata kitu?
5 Je, mtego bila chamboutamnasa ndege?Je, mtego hufyatukabila kuguswa na kitu?
6 Je, baragumu ya vita hulia mjinibila kutia watu hofu?Je, mji hupatwa na jangaasilolileta Mungu?
7 Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitubila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake.
8 Simba akinguruma,ni nani asiyeogopa?Bwana Mwenyezi-Mungu akinena,ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?
9 Tangazeni katika ikulu za Ashdodi,na katika ikulu za nchi ya Misri:“Kusanyikeni kwenye milimainayoizunguka nchi ya Samaria,mkajionee msukosuko mkubwana dhuluma zinazofanyika humo.”