5 Mnajisemea mioyoni mwenu:“Sikukuu ya mwezi mwandamo itakwisha liniili tuanze tena kuuza nafaka yetu?Siku ya Sabato itakwisha liniili tupate kuuza ngano yetu?Tutatumia vipimo hafifu vya wastani na uzito,tutadanganya watu kwa mizani isizo sawa,
6 hata kuuza ngano hafifu kwa bei kubwa.Tutaweza kununua watu fukara kwa fedha,na wahitaji kwa jozi ya kandambili.”
7 Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa:“Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.
8 Kwa hiyo, dunia itatetemekana kila mtu nchini ataomboleza.Nchi yote itayumbayumba;itapanda na kushuka,kama yanavyojaa na kupwa maji ya mto Nili!”
9 Bwana Mwenyezi-Mungu asema,“Siku hiyo nitalifanya jua litue adhuhuri,na kuijaza nchi giza mchana.
10 Sherehe zenu nitazigeuza kuwa kilio,na nyimbo zenu za furaha kuwa maombolezo.Nitawafanya nyote mvae magunia kwa huzunina kunyoa vipara vichwa vyenu,kama kuomboleza kifo cha mtoto wa pekee;na siku ya mwisho itakuwa ya uchungu mkubwa.”
11 Bwana Mwenyezi-Mungu asema,“Siku zaja ambapo nitaleta njaa nchini.Lakini sio njaa na kiu ya chakula na maji,bali njaa ya kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu.