1 Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,
2 “Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, utalisimika hema takatifu la mkutano.
3 Ndani ya hema hilo utaweka lile sanduku la ushuhuda, kisha weka pazia mbele yake.
4 Utaiingiza meza na kupanga vyombo vyake juu. Utaingiza kile kinara pia na kuziweka taa zake juu yake.