1 Afadhali kuwa na sifa nzuri kuliko mali nyingi;wema ni bora kuliko fedha au dhahabu.
2 Matajiri na maskini wana hali hii moja:Mwenyezi-Mungu ni Muumba wao wote.
3 Mtu mwangalifu huona hatari akajificha,lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia.
4 Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.