14 pamoja na ndugu zao; wote wakiwa 128, watu mashujaa. Na mkuu wao alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.
15 Nao Walawi waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, na mwana wa Buni.
16 Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu,
17 na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mzawa wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba sala za shukrani. Bakbukia alikuwa msaidizi wake. Pamoja nao alikuwako Abda, mwana wa Shamua, mwana wa Galali na mzawa wa Yeduthuni.
18 Walawi wote waliokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu, walikuwa 284.
19 Wangoja malango waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Akubu na Talmoni pamoja na ndugu zao waliokuwa wakilinda malango, walikuwa 172.
20 Watu wengine wa Israeli, makuhani na Walawi walikaa katika miji ya Yuda, kila mmoja katika urithi wake.