23 Mfalme alikuwa ametoa amri kuhusu zamu zao na mahitaji yao ya kila siku.
24 Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa mwakilishi kwa mfalme kuhusu mambo yote ya watu wa Yuda.
25 Watu wengine walikaa katika miji karibu na mashamba yao. Baadhi ya watu wa kabila la Yuda walikaa Kiriath-arba, Diboni na Yekabzeeli pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
26 Wengine pia walikaa katika miji ya Yeshua, Molada, Beth-peleti,
27 Hasar-shuali na Beer-sheba pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
28 Wengine walikaa katika mji wa Ziklagi, Mekona na vijiji vilivyoizunguka.
29 Wengine walikaa katika miji ya Enrimoni, Sora, Yarmuthi,