22 Wakati wa Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua wakuu wa jamaa za Walawi, waliorodheshwa; vilevile wakati wa utawala wa mfalme Dario wakuu wa jamaa za makuhani waliorodheshwa.
23 Wakuu wa jamaa za ukoo wa Lawi waliorodheshwa katika kitabu cha Kumbukumbu mpaka wakati wa Yohanani mjukuu wa Eliashibu.
24 Viongozi wa Walawi: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli walisimama mkabala na ndugu zao; walipangwa kuimba nyimbo za kusifu na kushukuru, kufuatana na amri ya mfalme Daudi, mtu wa Mungu.
25 Mabawabu walikuwa: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu; pia hao walikuwa walinzi wa ghala.
26 Watu hao waliishi wakati wa Yoyakimu, mwana wa Yeshua mwana wa Yosadaki na pia wakati wa Nehemia aliyekuwa mtawala wa mkoa; na hata wakati wa Ezra kuhani na mwandishi.
27 Kisha wakati wa kuweka wakfu ukuta wa Yerusalemu Walawi walitafutwa kila mahali walipokaa ili kuja Yerusalemu kusherehekea kwa furaha pamoja na shukrani na nyimbo, wakitumia matoazi, vinubi na zeze.
28 Wazawa wa waimbaji wakakusanyika kutoka viunga vya Yerusalemu na vijiji vya Wanetofathi,