4 Ataziweka hizo taa katika kinara cha taa cha dhahabu safi ziwake daima mbele ya Mwenyezi-Mungu.
5 “Chukua unga laini, kilo kumi na mbili na kuoka mikate kumi na miwili.
6 Mikate hiyo itapangwa safu mbili juu ya meza ya dhahabu safi, kila safu mikate sita.
7 Kila safu utaitia ubani safi ili iambatane na mikate hiyo, na kuwa sehemu ya sadaka ya kuteketezwa ya ukumbusho kwa Mwenyezi-Mungu.
8 Kila siku ya Sabato Aroni ataipanga sawasawa katika safu mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu kwa niaba ya watu wa Israeli kama agano la milele.
9 Aroni na wazawa wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo kwani ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.”
10 Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri.