5 Huyo kuhani, aliyepakwa mafuta atachukua kiasi cha damu na kuingia nayo ndani ya hema la mkutano.
6 Atachovya kidole chake katika damu hiyo na kuirashia mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu upande wa mbele wa pazia la mahali patakatifu.
7 Kuhani atachukua sehemu ya damu na kuzipaka pembe za madhabahu ya kufukizia ubani wa harufu nzuri, mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyoko karibu na mlango wa hema la mkutano.
8 Kisha atayaondoa mafuta yote ya ng'ombe huyo: Mafuta yanayofunika matumbo,
9 figo mbili na mafuta yaliyo juu yake na yale yaliyo kiunoni, na yale yaliyoshikamana na figo na ini; hizi ni sehemu zilezile zinazoondolewa kwa mnyama wa sadaka ya amani.
10 Kuhani atazichukua na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka.
11 Lakini ngozi ya huyo ng'ombe, nyama, kichwa, miguu, matumbo na mavi yake,