8 Kisha atayaondoa mafuta yote ya ng'ombe huyo: Mafuta yanayofunika matumbo,
9 figo mbili na mafuta yaliyo juu yake na yale yaliyo kiunoni, na yale yaliyoshikamana na figo na ini; hizi ni sehemu zilezile zinazoondolewa kwa mnyama wa sadaka ya amani.
10 Kuhani atazichukua na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka.
11 Lakini ngozi ya huyo ng'ombe, nyama, kichwa, miguu, matumbo na mavi yake,
12 yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
13 “Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu
14 mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano.