1 Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika.Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua;ndiye awapaye watu mvua za rasharasha,na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
2 Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu,na waaguzi wao wanaagua uongo;watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu,na kuwapa watu faraja tupu.Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo;wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,nami nitawaadhibu hao viongozi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4 Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:Watawala wa kila namna,viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,walio thabiti kama kigingi cha hema,wenye nguvu kama upinde wa vita.
5 Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitaniwatawakanyaga maadui zao katika tope njiani.Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;nao watawaaibisha hata wapandafarasi.