5 Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa,nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu;hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka.Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake,nao Ashkeloni hautakaliwa na watu.
6 Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kiburi cha Filistia nitakikomesha.
7 Nitawakomesha kula nyama yenye damu,na chakula ambacho ni chukizo.Mabaki watakuwa mali yangu,kama ukoo mmoja katika Yuda.Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi.
8 Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu,nitazuia majeshi yasipitepite humo.Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu,maana, kwa macho yangu mwenyewe,nimeona jinsi walivyoteseka.”
9 Shangilieni sana enyi watu wa Siyoni!Paazeni sauti, enyi watu wa Yerusalemu!Tazama, mfalme wenu anawajieni,anakuja kwa shangwe na ushindi!Ni mpole, amepanda punda,mwanapunda, mtoto wa punda.
10 Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu,na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu;pinde za vita zitavunjiliwa mbali.Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa;utawala wake utaenea toka bahari hata bahari,toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
11 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa sababu ya agano langu nanyi,agano lililothibitishwa kwa damu,nitawakomboa wafungwa wenuwalio kama wamefungwa katika shimo tupu.