29 Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote,Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika;Maana katika shina la nyoka atatoka fira,Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7
30 Nao walio maskini kabisa watakula,Na wahitaji watajilaza salama;Nami nitatia shina lako kwa njaa,Na mabaki yako watauawa.
31 Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji;Ee Ufilisti, pia wote, umeyeyuka kabisa;Maana moshi unakuja toka kaskazini,Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.
32 Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake wataona kimbilio.