1 Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa,Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;
2 Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari,Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji.Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini;Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,Ambao mito inakata nchi yao.
3 Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.
4 Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno.
5 Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
6 Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na hayawani wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na hayawani wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi.
7 Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini;Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,Ambao mito inakata nchi yao;Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.