14 Waleteeni wenye kiu maji,Enyi wenyeji wa nchi ya Tema;Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
15 Kwa maana wanakimbia mbele ya panga,Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa,Na mbele ya ukali wa vita.
16 Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.
17 Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.