10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu;Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
11 Nalisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai;Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
12 Kao langu limeondolewa kabisa,limechukuliwa kama hema ya mchungaji;Nimekunja maisha yangu kama mfumaji;atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
13 Nalijituliza hata asubuhi;kama simba, aivunja mifupa yangu yote;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
14 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia;Naliomboleza kama hua;macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu;Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
15 Niseme nini? Yeye amenena nami,na yeye mwenyewe ametenda hayo;Nitakwenda polepole miaka yangu yote,kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
16 Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote;Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.