7 Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa BWANA, ya kuwa BWANA atalitimiza jambo hili alilolisema;
8 Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.
9 Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.
10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu;Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
11 Nalisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai;Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
12 Kao langu limeondolewa kabisa,limechukuliwa kama hema ya mchungaji;Nimekunja maisha yangu kama mfumaji;atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
13 Nalijituliza hata asubuhi;kama simba, aivunja mifupa yangu yote;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.