15 Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
17 Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.
18 Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
19 Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.