14 umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako.
15 Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa BWANA, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo.
16 Hata itakuwa, akikuambia, Siondoki kwako; kwa sababu akupenda wewe na nyumba yako, kwa kuwa yu hali njema kwako;
17 ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo.
18 Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
19 Wazaliwa wa kwanza waume wote wazaliwao katika kundi lako la ng’ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.
20 Utamla mbele za BWANA, Mungu wako, mwaka hata mwaka mahali atakapochagua BWANA, wewe na nyumba yako.