1 BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo.
3 Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
4 Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
5 Naye atamchinja huyo ng’ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania