17 Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.
18 Basi, BWANA asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
19 Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.
20 Haya panda Lebanoni, ukalieUpalize sauti yako katika Bashani;Ukalie kutoka Abarimu;Maana wapenzi wako wote wameangamia.
21 Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.
22 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.
23 Wewe ukaaye Lebanoni,Ufanyaye kioto chako katika mierezi,Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana,Upatapo utungu kama wa mwanamke azaaye.