8 Misri anajiinua kama mto Nile,Na maji yake yanajirusha kama mito;Asema, Nitajiinua, nitaifunikiza nchi;Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake.
9 Haya! Pandeni, enyi farasi;Jihimizeni, enyi magari ya vita;Mashujaa nao na watoke njeKushi na Puti, watumiao ngao;Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.
10 Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi,Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake;Nao upanga utakula na kushiba,Utakunywa damu yao hata kukinai;Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yakeKatika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.
11 Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.
12 Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.
13 Neno hili ndilo ambalo BWANA alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadreza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri.
14 Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tahpanesi; semeni, Simama, ujifanye tayari kwa maana upanga umekula pande zako zote.