2 Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njoni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
3 Sauti ya kilio toka Horonaimu,Ya kutekwa na uharibifu mkuu.
4 Moabu umeharibika;Wadogo wake wamewasikiza watu kilio.
5 Kwa maana watu wapandapo huko LuhithiWatapanda wasiache kulia;Nao watu watelemkapo huko HoronaimuWameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.
6 Haya! Kimbieni! Jiokoeni nafsi zenu!Mkawe kama mtu aliye mkiwa.
7 Maana, kwa kuwa umeyatumainia matendo yako, na hazina zako, wewe nawe utatwaliwa; na Kemoshi atatoka aende katika uhamisho, makuhani wake na wakuu wake pamoja.
8 Naye mwenye kuteka nyara atakuja juu ya kila mji, wala hapana mji utakaookoka; bonde nalo litaangamia, nayo nchi tambarare itaharibiwa; kama BWANA alivyosema.