12 Maana BWANA asema hivi, Tazama, wale wasioandikiwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa.
13 Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
14 Nimepata habari kwa BWANA,Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa,Akisema, Jikusanyeni, mkaujie,Mkainuke kwenda vitani.
15 Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa,Na kudharauliwa katika watu.
16 Katika habari za kuogofya kwako,Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,Wewe ukaaye katika pango za majabali,Ushikaye kilele cha milima;Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai,Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
17 Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.
18 Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.