41 Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.
42 Wanashika upinde na mkuki;Ni wakatili, hawana huruma;Sauti yao inanguruma kama bahari,Nao wamepanda farasi;Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani,Juu yako, Ee binti Babeli.
43 Mfalme wa Babeli amesikia habari zao,Na mikono yake imekuwa dhaifu;Dhiki imemshika, na maumivu,Kama ya mwanamke katika utungu wake.
44 Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
45 Basi, lisikieni shauri la BWANA,Alilolifanya juu ya Babeli;Na makusudi yake aliyoyakusudiaJuu ya nchi ya Wakaldayo.Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi;Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
46 Kwa mshindo wa kutwaliwa Babeli nchi yatetemeka,Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.