4 Nao wataanguka, hali ya kuuawa, katika nchi ya Wakaldayo, hali ya kutumbuliwa katika njia kuu zake.
5 Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
6 Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
7 Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
8 Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.
9 Tungependa kuuponya Babeli,Lakini haukuponyeka;Mwacheni, nasi twendeni zetu,Kila mtu hata nchi yake mwenyewe;Maana hukumu yake inafika hata mbinguni,Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni.
10 BWANA ameitokeza haki yetu;Njoni, tutangaze katika SayuniHabari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.