52 Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataugua.
53 Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
54 Sauti ya kilio kutoka Babeli,Na ya uangamivu mkuu toka nchi ya Wakaldayo!
55 Maana BWANA amwangamiza Babeli,Na kuikomesha sauti kuu ndani yake;Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi,Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;
56 Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake;Naam, amefika Babeli;Na mashujaa wake wametwaliwa;Pinde zao zimevunjika kabisa;Maana BWANA ni Mungu wa kisasi;Hakika yake yeye atalipa.
57 Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
58 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.