26 Kwa hiyo, Walawi hawatahitaji tena kulibeba hema takatifu au vyombo vyake vya ibada.”
27 Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa.
28 Lakini wajibu wao ulikuwa ni kuwasaidia makuhani wa ukoo wa Aroni katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu; kuzitunza nyua na vyumba, kuvisafisha vyombo vitakatifu vyote na kufanya kazi zinazohusu huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
29 Pamoja na hayo, walisaidia katika kazi ya mikate mitakatifu, unga mwembamba na sadaka ya nafaka, maandazi yasiyotiwa chachu, sadaka iliyookwa; sadaka iliyochanganywa na mafuta; pia sadaka katika kazi ya upimaji wa wingi wa sadaka na ukubwa wake
30 na walisimama kumshukuru na kumsifu Mwenyezi-Mungu kila siku asubuhi na jioni,
31 na wakati wa siku za Sabato, mwezi mwandamo na sikukuu, hapo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Mwenyezi-Mungu. Sheria ziliwekwa kuhusu idadi ya Walawi walioagizwa kufanya kazi hizo daima mbele ya Mwenyezi-Mungu.
32 Kwa hiyo, ulikuwa ni wajibu wao kutunza hema la mkutano na mahali patakatifu, na kuwasaidia ndugu zao makuhani, wazawa wa Aroni, kwenye ibada katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.