14 Tafuteni kutenda mema na si mabaya,ili nyinyi mpate kuishinaye Mwenyezi-Mungu wa majeshiawe pamoja nanyi kama mnavyosema.
15 Chukieni uovu, pendeni wema,na kudumisha haki mahakamani.Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.
16 Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi,naam, Mwenyezi-Mungu asema:“Patakuwa na kilio kila mahali mitaani;watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’Wakulima wataitwa waje kuomboleza,na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
17 Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu;maana nitapita kati yenu kuwaadhibu.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.”
18 Ole wenu nyinyi mnaoingojea kwa hamusiku ya Mwenyezi-Mungu!Kwa nini mnaitaka sana siku hiyo?Siku hiyo, itakuwa siku ya giza na sio ya mwanga!
19 Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba,halafu akakumbana na dubu!Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake,akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
20 Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;itakuwa huzuni bila uangavu wowote.