1 Ole wenu nyinyi mnaostarehe huko Siyoni,nanyi mnaojiona salama mlimani Samaria!Nyinyi mwaonekana kuwa viongozi wa taifa maarufuambao Waisraeli wote huwategemea.
2 Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali,tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi,kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti.Je, falme zao si bora kuliko zenuna eneo lao si bora kuliko lenu?”
3 Nyinyi mnajaribu kuifukuza siku mbaya.Lakini mnauleta karibu utawala dhalimu.
4 Ole wenu mnaolala juu ya vitanda vya pembe za ndovuna kujinyosha juu ya masofa,mkila nyama za wanakondoo na ndama!
5 Nyinyi mnapenda kuimba ovyo na sauti ya vinubina kubuni ala mpya za muziki mkimwiga mfalme Daudi.
6 Mnakunywa divai kwa mabakuli,na kujipaka marashi mazuri mno.Lakini hamhuzuniki hata kidogojuu ya kuangamia kwa wazawa wa Yosefu.
7 Kwa hiyo mtakuwa wa kwanza kwenda uhamishoni,na karamu za wenye kustarehe zitatoweka.