1 Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Niliona kikapu kilichojaa matunda ya kiangazi.
2 Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli.Sitavumilia tena maovu yao.
3 Siku hiyo, nyimbo za ikulu zitakuwa maombolezo.Kutakuwa na maiti nyingi,nazo zitatupwa nje kimyakimya.”
4 Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyongena kuwaletea maangamizi fukara wa nchi.
5 Mnajisemea mioyoni mwenu:“Sikukuu ya mwezi mwandamo itakwisha liniili tuanze tena kuuza nafaka yetu?Siku ya Sabato itakwisha liniili tupate kuuza ngano yetu?Tutatumia vipimo hafifu vya wastani na uzito,tutadanganya watu kwa mizani isizo sawa,
6 hata kuuza ngano hafifu kwa bei kubwa.Tutaweza kununua watu fukara kwa fedha,na wahitaji kwa jozi ya kandambili.”
7 Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa:“Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.