11 Bwana Mwenyezi-Mungu asema,“Siku zaja ambapo nitaleta njaa nchini.Lakini sio njaa na kiu ya chakula na maji,bali njaa ya kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu.
12 Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari,kutoka upande wa kaskazini mpaka mashariki.Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Mwenyezi-Mungu,lakini hawatalipata.
13 “Siku hiyo, hata vijana wenye afya,wa kiume kwa wa kike,watazimia kwa kiu.
14 Wale wanaoapa kwa mungu wa uongo wa Samaria,na kusema: ‘Kwa nafsi ya mungu wako ee Dani’;na, ‘Kwa nafsi ya mungu wa Beer-sheba’,wote wataanguka na hawatainuka tena kamwe.”