1 Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama kando ya madhabahu, naye akaniamuru:“Zipige hizo nguzo za hekalumpaka misingi yake itikisike.Zivunje hizo nguzo ziwaangukie watu vichwani.Wale watakaosalia nitawaua kwa upanga;hakuna hata mmoja wao atakayenusurika,naam, hakuna atakayetoroka.
2 Wajapojichimbia njia ya kwenda kuzimu,huko nitawachukua kwa mkono wangu;wajapopanda mbinguni,nitawaporomosha chini.
3 Wajapojificha juu ya mlima Karmeli,huko nitawasaka na kuwachukua;wajapojificha mbali nami vilindini mwa bahari,humo nitaliamuru joka la baharini liwaume.
4 Wajapochukuliwa mateka na adui zao,huko nitatoa amri wauawe kwa upanga.Nitawachunga kwa makini sananiwatendee mabaya na si mema.”
5 Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi,anaigusa ardhi nayo inatetemekana wakazi wake wanaomboleza;dunia nzima inapanda na kushukakama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri.
6 Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni,nayo dunia akaifunika kwa anga;huyaita maji ya bahari,na kuyamwaga juu ya nchi kavu.Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!
7 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli,hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi!Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete,na Waashuru kutoka Kiri,kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.