7 “Efraimu ni sawa na mfanyabiasharaatumiaye mizani danganyifu,apendaye kudhulumu watu.
8 Efraimu amesema,‘Mimi ni tajiri!Mimi nimejitajirisha!Hamna ubaya kupata faida.Hata hivyo, hilo si kosa!’”
9 Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri!Mimi nitakukalisha tena katika mahema,kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu,wakati wa sikukuu ya vibanda.
10 Mimi niliongea na manabii;ni mimi niliyewapa maono mengi,na kwa njia yao natangaza mpango wangu.
11 Huko Gileadi ni mahali pa dhambi;huko Gilgali walitambika fahali,kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
12 Yakobo alikimbia nchi ya Aramuakiwa huko alifanya kazi apate mke,akachunga kondoo ili apate mke.
13 Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri,na kwa nabii Mungu aliwahifadhi.