1 Waefraimu waliponena, watu walitetemeka;Waefraimu walikuwa na uwezo mkubwa huko Israeli,lakini walianza kumwabudu Baali, wakajiletea kifo.
2 Waefraimu wameendelea kutenda dhambi,wakajitengenezea sanamu za kusubu,sanamu zilizotengenezwa kwa ustadi wao,zote zikiwa kazi ya mafundi.Wanasema, “Haya zitambikieni!”Wanaume wanabusu ndama!
3 Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi,kama umande utowekao upesi;kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria,kama moshi unaotoka katika bomba.
4 Mwenyezi-Mungu asema:“Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu,ambaye niliwatoa nchini Misri;hamna mungu mwingine ila mimi,wala hakuna awezaye kuwaokoeni.
5 Ni mimi niliyewatunza mlipokuwa jangwani,katika nchi iliyokuwa ya ukame.
6 Lakini mlipokwisha kula na kushiba,mlianza kuwa na kiburi, mpaka mkanisahau.
7 Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote;nitawavizieni kama chui njiani.
8 Nitawarukieni kama dubualiyenyang'anywa watoto wake.Nitawararua vifua vyenuna kuwala papo hapo kama simba;nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.
9 “Nitawaangamiza, enyi Waisraeli.Nani ataweza kuwasaidia?
10 Yuko wapi sasa mfalme wenu awaokoe?Wako wapi wale wakuu wenu wawalinde?Nyinyi ndio mlioomba:‘Tupatie mfalme na wakuu watutawale.’
11 Kwa hasira yangu mimi nikawapa mfalme,kisha nikamwondoa kwa ghadhabu yangu.
12 “Uovu wa Efraimu uko umeandikwa,dhambi yake imehifadhiwa ghalani.
13 Maumivu kama ya kujifungua mtoto yanamfikia.Lakini yeye ni mtoto mpumbavu;wakati ufikapo wa kuzaliwayeye hukataa kutoka tumboni kwa mama!
14 Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu;sharti niwaokoe kutoka kifoni!Ewe Kifo, yako wapi maafa yako?Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako?Mimi sitawaonea tena huruma!
15 “Hata kama Efraimu atastawi kama nyasi,mimi Mwenyezi-Mungu nitavumisha upepo wa mashariki,upepo utakaozuka huko jangwani,navyo visima vyake vitakwisha maji,chemchemi zake zitakauka.Hazina zake zote za thamani zitanyakuliwa.”
16 Watu wa Samaria wataadhibiwa kwa kosa lao.Kwa sababu wamemwasi Mungu wao.Watauawa kwa upanga,vitoto vyao vitapondwapondwa,na kina mama wajawazito watatumbuliwa.