Hosea 11 BHN

Upendo wa Mungu wapita hasira yake

1 “Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,Kutoka Misri nilimwita mwanangu.

2 Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita,ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami;waliendelea kuyatambikia Mabaali,na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu.

3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.

4 Niliwaongoza kwa kamba za hurumanaam, kwa kamba za upendo;kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,ndivyo nami nilivyokuwa kwao.Mimi niliinama chini na kuwalisha.

5 Basi, watarudi nchini Misri;watatawaliwa na mfalme wa Ashuru,kwa sababu wamekataa kunirudia.

6 “Upanga utavuma katika miji yao,utavunjavunja miimo ya malango yakena kuwaangamiza katika ngome zao.

7 Watu wangu wamepania kuniacha mimi,wakiitwa waje juu,hakuna hata mmoja anayeweza.

8 Ewe Efraimu, nawezaje kukuacha?Nawezaje kukutupa ewe Israeli?Nitawezaje kukufanya kama mji wa Adma?Nitawezaje kukutenda kama Seboimu!Nazuiwa na moyo wangu;huruma yangu imezidi kuwa motomoto.

9 Nitaizuia hasira yangu kali;sitamwangamiza tena Efraimu,maana mimi ni Mungu, wala si binadamu.“Mimi ndimi Mtakatifu miongoni mwenu,nami sitakuja kuwaangamiza.

10 “Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba;nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.

11 Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege,wataruka kutoka Ashuru kama huanami nitawarudisha makwao;mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

12 Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,na Waisraeli udanganyifu.Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14