1 “ ‘Twendeni, tukamrudie Mwenyezi-Mungu!Yeye mwenyewe ameturarua,lakini yeye mwenyewe atatuponya.Yeye mwenyewe ametujeruhi,lakini yeye mwenyewe atatibu majeraha yetu.
2 Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena,naam, siku ya tatu atatufufuaili tuweze kuishi pamoja naye.
3 Basi tumtambue,tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu.Kuja kwake ni hakika kama alfajiri,yeye atatujia kama manyunyu,kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
4 Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakutendea nini ee Efraimu?Nikufanyie nini ee Yuda?Upendo wenu kwangu ni kama ukungu wa asubuhi,kama umande unaotoweka upesi.
5 Ndiyo maana nimewavamia kwa njia ya manabii,nimewaangamiza kwa maneno yangu,hukumu yangu huchomoza kama pambazuko.
6 Maana ninachotaka kwenu ni upendo na si tambiko,Kumjua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa.
7 “Lakini mlilivunja agano langukama mlivyofanya mjini Adamu;huko walinikosea uaminifu.
8 Gileadi ni mji wa waovu,umetapakaa damu.
9 Kama wanyang'anyi wamwoteavyo mtu njiani,ndivyo na makuhani walivyojikusanya na kuvizia.Wanaua watu njiani kuelekea Shekemu,naam, wanatenda uovu kupindukia.
10 Nimeona jambo la kuchukiza sanamiongoni mwa Waisraeli:Watu wa Efraimu wanakimbilia miungu minginenaam, Waisraeli wamejitia unajisi.
11 Nawe Yuda hali kadhalika,nimekupangia wakati utakapovuna adhabu.