1 “Haya! Sikilizeni enyi makuhani!Tegeni sikio, enyi Waisraeli!Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme!Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki,badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa,mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
2 Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu.Lakini mimi nitawaadhibuni nyote.
3 Nawajua watu wa Efraimu,Waisraeli hawakufichika kwangu.Nyinyi watu wa Efraimu mmefanya uzinzi,watu wote wa Israeli wamejitia najisi.
4 “Matendo yao yanawazuia wasimrudie Mungu wao.Mioyoni mwao wamejaa uzinzi;hawanijui mimi Mwenyezi-Mungu.
5 Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi;watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao,nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao.
6 Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe,kumtafuta Mwenyezi-Mungu;lakini hawataweza kumpata,kwa sababu amejitenga nao.
7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu,wamezaa watoto walio haramu.Mwezi mwandamo utawaangamiza,pamoja na mashamba yao.
8 “Pigeni baragumu huko Gibea,na tarumbeta huko Rama.Pigeni king'ora huko Beth-aveni.Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!
9 Siku nitakapotoa adhabuEfraimu itakuwa kama jangwa!Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10 Viongozi wa Yuda wamekuwawenye kubadili mipaka ya ardhi.Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11 Efraimu ameteswa,haki zake zimetwaliwa;kwani alipania kufuata upuuzi.
12 Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu,kama donda baya kwa watu wa Yuda.
13 Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao,naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao,watu wa Efraimu walikwenda Ashurukuomba msaada kwa mfalme mkuu;lakini yeye hakuweza kuwatibu,hakuweza kuponya donda lenu.
14 Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu,kama mwanasimba kwa watu wa Yuda.Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka,nitawachukua na hakuna atakayewaokoa.
15 Nitarudi mahali pangu na kujitenga naompaka wakiri kosa lao na kunirudia.Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema: