16 Waisraeli ni wakaidi kama punda.Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga,kama kondoo kwenye malisho mapana?
17 “Watu wa Efraimu wamejifunga na sanamu.Haya! Waache waendelee tu!
18 Kama vile genge la walevi,wanajitosa wenyewe katika uzinzi;wanapendelea aibu kuliko heshima yao.
19 Basi, kimbunga kitawapeperusha,na watayaonea aibu matambiko yao kwa miungu ya uongo.