1 Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu,ninapotaka kuwaponya Waisraeli,uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa,matendo mabaya ya Samaria hujitokeza.Wao huongozwa na udanganyifu,kwenye nyumba wezi huvunjanje barabarani wanyang'anyi huvamia.
2 Hawafikiri hata kidogo kwamba miminayakumbuka maovu yao yote.Sasa maovu yao yamewabana.Yote waliyotenda yako mbele yangu.
3 “Wanamfurahisha mfalme kwa maovu yaowanawafurahisha wakuu kwa uhaini wao.
4 Wote ni wazinzi;wao ni kama tanuri iliyowashwa motoambao mwokaji hauchochei tangu akande ungampaka mkate utakapoumuka.
5 Kwenye sikukuu ya mfalme,waliwalewesha sana maofisa wake;naye mfalme akashirikiana na wahuni.
6 Kama tanuri iwakavyo,mioyo yao huwaka kwa hila;usiku kucha hasira yao hufuka moshi,ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.