5 Kwenye sikukuu ya mfalme,waliwalewesha sana maofisa wake;naye mfalme akashirikiana na wahuni.
6 Kama tanuri iwakavyo,mioyo yao huwaka kwa hila;usiku kucha hasira yao hufuka moshi,ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.
7 Wote wamewaka hasira kama tanuri,na wanawaangamiza watawala wao.Wafalme wao wote wameanguka,wala hakuna anayeniomba msaada.
8 “Efraimu amechanganyika na watu wa mataifa.Anaonekana kama mkate ambao haukugeuzwa.
9 Wageni wamezinyonya nguvu zake,wala yeye mwenyewe hajui;mvi zimetapakaa kichwani mwake,lakini mwenyewe hana habari.
10 Kiburi cha Waisraeli chashuhudia dhidi yao,hawanirudii mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao;wala hawanitafuti kwa matukio hayo yote.
11 Efraimu ni kama njiwa, mjinga asiye na akili;mara yuko Misri, mara Ashuru kuomba.