15 Wakuu wa Edomu wamefadhaishwa;viongozi wa Moabu wamekumbwa na woga mkuu;wakazi wote wa Kanaani wamevunjika moyo.
16 Kitisho na hofu vimewavamia.Kwa sababu ya ukuu wa nguvu zako,wao wamenyamaza kimya kama jiwe,mpaka watu wako ee Mwenyezi-Mungu, wapite,naam, mpaka watu hao uliowakomboa wamewapita.
17 Wewe utawaleta watu wako na kuwapanda mlimani pako;pale ulipochagua ee Mwenyezi-Mungu pawe makao yako,mahali patakatifu ee Mwenyezi-Mungu ulipojenga kwa mikono yako.
18 Wewe, ee Mwenyezi-Mungu,watawala milele na milele.”
19 Wakati farasi wa Farao na magari yake pamoja na wapandafarasi wake walipoingia mahali pakavu baharini, Mwenyezi-Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.
20 Basi nabii Miriamu, dada yake Aroni, akachukua kingoma mkononi, na wanawake wengine wote wakamfuata wakiwa na vingoma vyao wakicheza.
21 Miriamu akawaongoza kwa kuimba,“Mwimbieni Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari,farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.”