1 “Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya.
2 Usifuate genge la watu kutenda uovu, wala usijumuike na genge la watu kutoa ushahidi mahakamani ili kupotosha haki.
3 Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini.
4 “Ukimkuta ng'ombe au punda wa adui yako amepotea, utamrudishia mwenyewe.
5 Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
6 “Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake.
7 Jitenge mbali na mashtaka ya uongo wala usiwaue wasio na hatia na waadilifu, maana mimi sitamsamehe mtu mwovu.