3 Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini.
4 “Ukimkuta ng'ombe au punda wa adui yako amepotea, utamrudishia mwenyewe.
5 Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
6 “Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake.
7 Jitenge mbali na mashtaka ya uongo wala usiwaue wasio na hatia na waadilifu, maana mimi sitamsamehe mtu mwovu.
8 Usipokee rushwa, maana rushwa huwapofusha wakuu na kupotosha mambo ya wenye haki.
9 “Usimdhulumu mgeni; nyinyi mwajua hali ya kuwa mgeni, maana mlikuwa wageni nchini Misri.