1 “Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.
2 Katika kila pembe ya madhabahu hiyo utatengeneza upembe ambao utakuwa umeundwa kutokana na madhabahu yenyewe. Madhabahu hiyo yote utaipaka shaba.
3 Utaitengenezea vyombo vyake: Vyungu vya majivu, sepetu, na mabirika, na nyuma na visahani vya kuchukulia moto. Vyombo vyake vyote utavitengeneza kwa shaba.
4 Kisha utatengeneza wavu wa shaba wenye pete nne za shaba kwenye pembe zake nne.
5 Wavu huo utauweka kwenye ukingo wa madhabahu upande wa chini ili ufike katikati ya madhabahu.
6 Utatengeneza pia mipiko ya mjohoro ya kuibebea madhabahu; nayo utaipaka shaba.
7 Mipiko hiyo itaingizwa kwenye zile pete kila upande wa madhabahu, wakati wa kuibeba.